RiffVibe

Chama cha Kalonzo chataka kumpokonya mwandani wa Raila cheo alichopewa bungeni

- Chama cha Kalonzo Musyoka kimetaka nafasi ya naibu wa kiranja wa wachache katika bunge kipewe mbunge wa Kathiani Robert Mbui

-Chama hicho pia kilitaka orodha ya wabunge na nafasi walizokuwa wamepewa kuwasilishwa upya bungeni Kalonzo akiwa

- Naibu kiongozi wa chama hicho, Kivutha Kibwana alisema kuwa mbunge wa suna Mashariki,Junnet Mohammed ambaye ameshikilia nafasi hiyo,anapaswa kuivua na kumpa Mbui

Mvutano unazidi kushuhudiwa katika muungano wa NASA huku viongozi wakizozania nafasi kadhaa katika bunge.

Habari Nyingine: Prezzo akutana na bintiye baada miaka, furaha yake haifichiki(video)

Habari Nyingine: 2018 ni mwaka wa kuibadilisha Kenya na kuifanya Canaan- Raila

Chama cha Kalonzo Musyoka cha Wiper kimelalama kuhusu nafasi nono kupewa viongozi wa vyama vingine tanzu huku viongozi wa chama hicho wakipuuza.

Sasa kimetaka nafasi ya naibu kiranja wa wachache katika bunge ipewe mbunge wa Kathiani Robert Mbui.

Viongozi wa Wiper wakiongozwa na Kivutha Kibwana,walimtaka mbunge wa Suna Mashariki ambaye sasa anashikilia kiti hicho kukivua na kumpatia mbui.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Mume asiyependa kuoga aachwa na mkewe siku chache baada ya harusi

Itakumbukwa kuwa ,Septemba 2017,viongozi wa muungano wa NASA waliteua viongozi ambao wangewasilisha muungano huo katika bunge la seneti na bunge la kitaifa.

Aidha uteuzi huo haukuwaridhisha baadhi ya viongozi kutoka mkoa wa Pwani kwani walidai kubaguliwa na hata walitishia kung'atuka kwenye muungano huo.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia394f5FmmqGZnZZ6pLTAZqKapJ%2Bjx7B5wqGYrZmblnqswcyppqSnnq6ubrnWmqWdmZ6eeritjKuYoqSRYrCpsc5mmKWhk528sbHWmmSbrZ6csq%2B1jaGrpqQ%3D

Larita Shotwell

Update: 2024-07-07